Leo napenda kuongelea Faida azipatazo mama na mtoto pale mama
anapochukua jukumu la kumnyonyesha mtoto vyema na kwa muda uliopangwa ,
Najua siku hizi kina dada kina mama wengi wamekimbilia
utandawazi wanaogopa kuwanyonyesha watoto wao kwa kuogopa ,Matiti kuanguka na kupoteza umbo lake
la asilia kitu ambacho si sahahi kabisa kwani
mtoto anatakiwa kupata haki yake ya msingi.
Lakini tukirudi katika ukweli asilia kwa nini mama anabeba
mimba miezi tisa,Na Mama akijifungua
maziwa yanakuwa tayari yametengenezwa tayari kwa ajili ya chakula cha mtoto
,Ndipo tutarudi katika imani zaidi kuwa mwenyezi mungu alikuwa na maana yake
kuanzia uumbaji wa mtoto mpaka kujifungua kwa mama
Ni ni haki ya mtoto ya msingi kupata maziwa ya mama,
Mbali na kumpa mtoto
chakula pale anaponyonyeshwa vizuri kwa kufata utaratibu ,inajenga Bond au
ukaribu wa mama na mtoto,Mie huwa nasikia rah asana pale mwanangu
anapoanza kupata utambuzi na kunyonya huku akikutizama usoni ,akirusha
rusha miguu yake na wakati mwingi anakushika kidevu kwa Furaha ,Ni tendo
la ajabu na la Furaha huwa najisikia kucheka kwa sana na kusikia nguvu Fulani ndani ya
mwili wangu.na kujisikia kweli nimezaa na sasa namnyonyesha mwanangu
niliye mtoa ndani ya tumbo LANGU-
NI VYEMA MAMA AMNYONYESHE MWANAE ILI KUJENGA UKARIBU WA MAMA NA MTOTO
Pia maziwa ya mama yana
afya na vitamin zote ,maziwa ya mama yanamsaidia mtoto kuepuka magonjwa
ambayo yanaweza kuzuilika ,Na imani kabisa maziwa ya mama yanafanya Ubongo
wa mtoto uwe active na kumjenga kiakili. Nawasisitiza kina mama wote
waendelee kunyonyesha watoto wao kwa muda wote unaostahiri mtoto kunyonya
,na kuepukana na hofu ya kupoteza uhalisia wa umbo zima la matiti yao.
Pia unapunguza gharama
za kuanza kununua maziwa ya makopo au ya ng’ombe ya kukamua kwa kipindi chote cha mwanzo utakachokuwa
unamnyonyesha mtoto,
BADO NAENDELEA KUSISITIZA
WAKINAMAMA KUNYONYESHA KWANI INAJENGA UHUSIANO MZURI WA MAMA NA MTOTO PALE
UNAPOMPAKATA NA KUMPA MAZIWA KUTOKA KIFUANI MWAKO MTOTO
|
Asante sana Janet
ReplyDeleteUmetoa post nzuri sana leo
i like it ,hongera na kwa wamama wote mjifunze ,mjue kuna faida kubwa kunyonyesha
ReplyDeleteasante Blogger ,wakina mama wote mpite huko
ReplyDeleteNilikuwa naogopa manyonyo kudondoka sasa nitanyonyesha umenigusa
ReplyDelete