Monday, January 6, 2014

Faida za Mama Kunyonyesha mtoto




Leo napenda kuongelea Faida azipatazo mama na mtoto pale mama anapochukua jukumu la kumnyonyesha mtoto vyema na kwa muda uliopangwa ,

Najua siku hizi kina dada kina mama wengi wamekimbilia utandawazi wanaogopa kuwanyonyesha watoto wao kwa  kuogopa ,Matiti kuanguka na kupoteza umbo lake la asilia kitu ambacho si sahahi kabisa kwani  mtoto anatakiwa kupata haki yake ya msingi.

Lakini tukirudi katika ukweli asilia kwa nini mama anabeba mimba miezi tisa,Na  Mama akijifungua maziwa yanakuwa tayari yametengenezwa tayari kwa ajili ya chakula cha mtoto ,Ndipo tutarudi katika imani zaidi kuwa mwenyezi mungu alikuwa na maana yake kuanzia uumbaji wa mtoto mpaka kujifungua kwa mama

Ni ni haki ya mtoto ya msingi kupata maziwa ya mama,

  1. Mbali na kumpa mtoto chakula pale anaponyonyeshwa vizuri kwa kufata utaratibu ,inajenga Bond au ukaribu wa mama na mtoto,Mie huwa nasikia rah asana pale mwanangu anapoanza kupata utambuzi na kunyonya huku akikutizama usoni ,akirusha rusha miguu yake na wakati mwingi anakushika kidevu kwa Furaha ,Ni tendo la ajabu na la Furaha huwa najisikia kucheka kwa  sana na kusikia nguvu Fulani ndani ya mwili wangu.na kujisikia kweli nimezaa na sasa namnyonyesha mwanangu niliye mtoa ndani ya  tumbo LANGU- NI VYEMA MAMA AMNYONYESHE MWANAE ILI KUJENGA UKARIBU WA MAMA NA MTOTO

  2. Pia maziwa ya mama yana afya na vitamin zote ,maziwa ya mama yanamsaidia mtoto kuepuka magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika ,Na imani kabisa maziwa ya mama yanafanya Ubongo wa mtoto uwe active na kumjenga kiakili. Nawasisitiza kina mama wote waendelee kunyonyesha watoto wao kwa muda wote unaostahiri mtoto kunyonya ,na kuepukana na hofu ya kupoteza uhalisia wa umbo zima la matiti yao.

  3. Pia unapunguza gharama za kuanza kununua maziwa ya makopo au ya ng’ombe  ya kukamua kwa kipindi chote cha mwanzo utakachokuwa unamnyonyesha mtoto,

BADO NAENDELEA KUSISITIZA WAKINAMAMA KUNYONYESHA KWANI INAJENGA UHUSIANO MZURI WA MAMA NA MTOTO PALE UNAPOMPAKATA NA KUMPA MAZIWA KUTOKA KIFUANI MWAKO MTOTO



4 comments:

  1. Asante sana Janet
    Umetoa post nzuri sana leo

    ReplyDelete
  2. i like it ,hongera na kwa wamama wote mjifunze ,mjue kuna faida kubwa kunyonyesha

    ReplyDelete
  3. asante Blogger ,wakina mama wote mpite huko

    ReplyDelete
  4. Nilikuwa naogopa manyonyo kudondoka sasa nitanyonyesha umenigusa

    ReplyDelete