Wednesday, November 13, 2013

Dear JFS:Nampenda mme wangu lakini hataki kuyapokea mapenzi yangu nifanyeje?

Pole na kazi dadaangu

Mie ni mama wa watoto wawili  wakike mmoja yuko 6 yrs na mmoja 1 yrs nimefunga ndoa na mme wangi miaka saba iliyopita,ninafanya kazi ,najipenda naipenda family yangu pia nampenda sana mme wangu na nimekuwa nikimuonyesha kwa vitendo kuwa nampenda
Tatizo lililonifanya nikuandikie ni hili ,baada ya miaka miwili ya ndoa yetu mme wangu amekuwa busy na mambo yake ,kurudi nyumbani usiku wa manane  amelewa,na akiwa huko alipoenda mpaka usiku wa manane  nikimpigia simu ananiambia anapajua nyumbani ..mwenzenu silali nakosa usingizi mpaka anaporudi nyumbani ndio naweza kupata usingizi japo kidogo  ,na  akiwa mbali nikimtumia meseji za kumwambia mme wangu nakupenda,mme wangu nakumiss ,nachojibu ni najua au asante ..Nashangaa mwenzenu maana nachotengemea ni nakupenda pia au nakumiss pia ,lakini yeye jibu ni "najua" ,Pia usipompigia saa nyingine usitegee yeye akupigie Linapokuja swala la matumizi ya ndani mpaka nimuombe hawezi sema huu mwisho wa mwezi nitoe hela kwa ajili ya matumizi ya family ,nakuomba omba sometimes inakuwa tabu ni mtu gani haya mtu  anakuwa hajui mahitaji ya familia yake
Nimekuwa mpweke mpaka naona kama nadhulumiwa penzi langu ,natamani  kusikia neno la nakumiss ,nakupenda pia .mme wangu ananifanya nianze kuwa mawazo mabaya
Nifanyeje wapenzi wangu naomba msaada wenu kimawazo
 Muathirika
Pls usiweke email yangu

Ushauri  wangu

Pole sana dada haya yote ni majatribu ya ndoa jaribu kuwashirikisha wasimamizi wa harusi yenu wamwite mkae na kutoa kero zinazokusumbua..inaweza kuwa msaada
***********************************************
Pia naimani wasomaji watakupa msaada zaidi kimawazo

Ukiwa na Maoni na ushauri Tuma kwenda Janetfands@gmail.com

9 comments:

  1. pole sana dada hivi ndoa ndo ngumu hivyo

    ReplyDelete
  2. majanga juu ya majanga enye waume wapendeni wake zenu

    ReplyDelete
  3. MMMMMMMMH HATARE WANAUME MKOJE ? MPENDWEJE?

    ReplyDelete
  4. Angemuacha hata week nzima bila sms kwake kama anavyonyamaza na yy anyamaze mwanaume wa siku ni majanga usipomuuliza kitu ataona huna time naye atajirudi wewe kaa hata mwezi mzima upunguze mapenzi uone atajirudi tu me wa kwangu alikuwa anaanza kubadilika na me nina kisirani cha kikurya basi na me kimya 2 days tu aliomba msamaha na tukasifiri mapenzi yakarudi kabla nililikuwa nikimtumia sms anakaa hata 3hours ndio anajibu nikasema unijue wewe nika mute 2 days aliomba msamaha

    ReplyDelete
    Replies
    1. naungana nawe mdau. jaribu kumpotezea japo hata mwezi tu. Ni ngumu lakini it is worth trying honey. yani kiukweli hii mada yako imeniuma utadhani nakufahamu. na kusema ukweli dunia ya sasa mapenzi yamekuwa kizungumkuti mno. wewe umefunguka lakini kuna watu mi nawafahamu unaambia hali ni mbaya kukuzidi, kwa kifupi tunazidiana tu hizi tabu za ndoa, wengine nje wanaonyesha ni happy couple lakini ndani kila mtu na chumba chake, wewe unajibiwa asante, wengine meseji zao hazijibiwi, simu zao hazipokelewi, au akipokea simu UTASIKI..SEMA UNA SHIDA GANI! sasa mtu akikuuliza hivi unapata picha sura yake ikoje aliposikia simu inaita kwenye screen inaonyesha wewe mkewe ndo unampigia, ndo mana mtaa wa pili kule kwnye kijiwe chetu kingine kuna mdau alisema yeye kamsevu wake mume wake "MSHENZI" ikifikia hatua hii jua wazi naye yameshamkuta mengi ya kukera ameona isiwe shida, anaendelea na maisha yake wakiwa mume na mke lakini upendo hapo hakuna. kwa hiyo, usiwe stressed up, keep yourself busy, usijiachie yani uwe una pendeza siku zote, hataki mitoko na wewe, we ikifika weekend andaa wanao, na kama una shogaako unayemwamini, tokeni mwende mahali mkaenjoy, kunywa kinywaji ukipendacho (sio kulewa) na unapokwenda out aga, ikiwezekana pendeza sana, livizie liko home linaangalia TV tokelezea na wanao hao.....akichelewa kurudi, asirudi, usiulize, pia usiache kumwekea chakula kama ndo desturi yako kumwekea, ka kifupi usiache duties za mke kama ilivyo kawaida yako.Good lucky mami

      Delete
  5. Pole sana Mwanamke mwenzetu ,yaani hili mbona janga kubwa mie wa kwangu sina hamu nae ,nikiwa mjamzito mimba miezi nane aaanza akitoka ndo harudi imagine na tumbo langu hapo BP za kugikia mwanaume humuoni yaani kila siku nilikuwa nakimbizwa Hospital Presha ingawa mwanzo nilikuwa nasema nimpetezee unajua ukiwa mjamzito uvumilivu unakuwa mdogo,nilijikuta nimejifungua siku si zangu.mpaka sasa nimemuweka mme wangu kipolo namtafutia maumivu na yeye..huu uzao wa adam mbona uko hivi kututesa tu jamani
    Najuuta kuolewa

    ReplyDelete
  6. pole sana dada inauma sana jamani ,naona kuna hao walokushauri umpotezee wamekupa ushari mzuri sana jaribu njia hizo inaweza kuwa ahueni kwako

    dunia imeingiliwa

    ReplyDelete
  7. Pole dada mie nakupa ushauri kama mwanaume inawezekana mmeo kapata mtu anayemzuzua huko njenhasa baada ya wewe kupata watoto ,hebu jicheki kama kuna mapungufu yoyote unayo tangu umejifungua ,bado unajitunza na kujipenda kama awali usafi wa mwili na nyumba chakula na watoto
    please twambie

    ReplyDelete
  8. Pole dear mungu akupiganie

    ReplyDelete