Monday, November 11, 2013

Leo tunamwangalia muigizaji wa Mexico mwenye Makeke anapouvaa uhusika Diana Sabine Moussier

Diana Sabine Moussier mwanamama machachali anayetamba kwenye tamthilia za Mexico,Napenda sana kumuona na pia naupenda sana uigizaji wake
Alizaliwa tarehe 23 August mwaka 1966 ni Mjerumani mwenye asili ya Mexico,na pia ni mama wa watoto wawili
Amekuwa akisifika katika uigizaji wake wa kikakitili na usaliti ndani ya ndoa na kuuvaa uhusika hasaa, na unaweza kumchukia akiwa katika kazi yake ya uigizaji
Ameigiza tamthilia nyingi sana na zilizompatia umaarufu hata kuweza kujipatia tuzo nchini mwake ,baadhi ya tamthilia alizoigiza ni Mi Pecado inayoonyeshwa kwa sasa katika kituo cha Capital Television,akiwa anatumia jina la Justina Almada ,picha imeigizwa 2009,2012 ameigiza picha Abisimo De Pasion inayoonyeshwa Citizen Channel ya Kenya akitumia jina la Carmina Bourvier ,2013 amecheza picha mpya Amores Verdaderos  akitumia jina la Bruna Cristo,Binafsi namkubali sana anapouvaa uhusika ,ni mkatili sana anapokuwa katika sehemu yake ..kwa wale wanaofuatilia tamthilia za kimexico..

No comments:

Post a Comment